Fatima Mohajerani amebainisha kuwa "Wizara ya Mambo ya Nje ilifafanua kwamba tarehe ya mazungumzo haijaainishwa, na inaweza kuwa si hivi karibuni, na hakuna uamuzi wowote ambao umechukuliwa kuhusiana na suala hili."
Mohajerani alidokeza kwamba wakati wa uchokozi wa hivi majuzi, adui Israel alilenga vituo kadhaa muhimu, vikiwemo: Hospitali za shahidi Motahhari, Khatam, Labafinejad, Farabi Kermanshah, Kituo cha Watoto Yatima katika Kasri la Shirin, na Kituo cha Hilali Nyekundu cha Kuhudumia Watu Wenye Mahitaji Maalumu.
Msemaji wa serikali ya Iran amesema kuwa idadi ya mashahidi imeongezeka na kufikia 935, wakiwemo wanawake na watoto 140 waliuawa shahidi katika vita vya utawala ghasibu wa Israel.
Mohajerani amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari alioufanya na kueleza kwamba, "Wakati wa uvamizi huo, tulishuhudia matukio machungu, ikiwa ni pamoja na mashambulizi kwenye jengo la redio na televisheni, gereza la Evin, hospitali, vitengo vya misaada na na kadhalika ... Ni watu wa aina gani wanaofanya vitendo hivi? Yalikuwa matukio magumu, lakini nchi yetu imejaa watu wenye ujasiri."
Msemaji wa serikali ya Iran ameongeza kusema kuwa, tangu dakika za mwanzo za uchokozi, serikali ilianza kazi yake, na Waziri wa Afya alikuwa wa kwanza kutekeleza majukumu yake, kwani vyumba vya dharura viliundwa kwa uratibu na vyuo vikuu vya sayansi ya matibabu.
342/
Your Comment